<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><hymn_number>108</hymn_number>
<lyrics>[V1]
 Mpendao Bwana
 Ije raha yenu!
 Imbeni nyimbo za raha
 Wa ibada yenu.

[V2]
 Twenenda Sayuni,
 Mji mzuri Sayuni;
 Twenenda juu Sayuni
 Ni maskani ya Mungu.

[V3]
 Wasiimbe wao
 wasioamini,
 Watoto wa Mungu ndio
 waimbao chini.

[V4]
 Twaona rohoni
 Baraka za Mungu,
 Tusijafika Mbinguni
 Kwenye utukufu.

[V5]
 Tutakapo mwona
 Masumbuko basi,
 Huwa maji ya uzima,
 Anasa halisi.

[V6]
 Tupaaze sauti,
 Na fute machozi,
 Twenenda kwa Imanweli
 Naye ni Mwokozi.</lyrics>
<title>Twenenda Sayuni TZR108</title>
</song>